Home Michezo Poland, Georgia na Ukraine zatinga kipute cha Euro 2024

Poland, Georgia na Ukraine zatinga kipute cha Euro 2024

0

Poland, Georgia na Ukraine ndizo timu tatu za mwisho kujikatia tiketi kwa fainali za mwaka huu za kombe la Euro kati ya Juni na Julai nchini Ujerumani.

Ukraine imejumuishwa kundi E la Euro pamoja na Ubelgiji, Slovakia na Romania baada ya kuwabandua Iceland mabao 2-1 katik mchujo wa Jumanne.

Poland ilifuzu baada ya kuwashinda wenyeji Wales kupitia penalti 5-4 katika mechi iliyosakatwa mjini Cardiff.

Pambano hilo lilikamilika kwa sare tasa huku wakifuzu kwa kipute cha Euro kwa mara ya 11.

Georgia pia wakiwa nyumbani waliweka historia kufuzu kwa fainali za Euro kwa mara ya kwanza walipowatema Ugiriki kupitia penalti 4-2 baada ya sare tasa.