Jumuiya ya Afrika Mashariki imeeleza nia na madhumuni yake ya kuunganisha nchi wanachama na kuhakikisha kuna amani na utulivu. Hata Hivyo katibu katika wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na maendeleo ya kikanda, Abdi Dubat ameeleza imani ya uwezo wa Jumuia hiyo kuvutia mataifa mengi katika kukuza biashara.