Home Habari Kuu Paul Mackenzie afungwa miezi 12 jela kwa kumiliki studio bila idhini

Paul Mackenzie afungwa miezi 12 jela kwa kumiliki studio bila idhini

Mhubiri wa kanisa la Good News International, Paul Mackenzie.

Mahakama ya Malindi leo Ijumaa imemhukumu mhubiri mwenye utata, Paul Mackenzie kifungo cha miezi 12 gerezani kwa kumiliki na kusambaza filamu ambazo hazijakaguliwa na kuainishwa na Bodi ya Filamu nchini.

Hakimu Mkuu wa Malindi Olga Juma Onalo pia alimhukumu kifungo cha miezi sita gerezani mhubiri huyo wa Kanisa la Good News International lililopigwa marufuku kwa kuendesha studio na kutayarisha filamu bila leseni.

Atatumika vifungo hivyo kwa wakati mmoja.

Akimhukumu Mackenzie, Onalo alisema alizingatia ukweli kwamba mfungwa huyo alikuwa na umri wa miaka 50 na mwenye kujuta. Alisema pia alikuwa amehama na kuuza kituo chake cha televisheni.

Hata hivyo, Onalo alibaini kuwa Mackenzie alikuwa amerudia kosa.

Alisema katika uamuzi wake kwamba mhubiri huyo mwenye alishtakiwa kwa kosa la kumiliki na kuonyesha filamu ambazo hazijakaguliwa na alipaswa kujiepusha kurudia kosa hilo.

Website | + posts
Radio Taifa
+ posts