Home Vipindi Paul Famba ateuliwa mkurugenzi mtendaji wa PSC

Paul Famba ateuliwa mkurugenzi mtendaji wa PSC

0
kra

Bwana Paul Famba ameteuliwa na tume ya utumishi wa umma PSC kuwa mkurugenzi mtendaji na katibu.

Uteuzi huo ulitangazwa kupitia ilani iliyofafanua kwamba atashikilia wadhifa huo kwa miaka mitano na kwamba tume hiyo ilitekeleza uteuzi huo kupitia kwa mamlaka iliyopatiwa na sehemu ya pili ya kifungu cha 15 cha sheria ya PSC.

kra

Hayo ni kulingana na mwenyekiti wa PSC Anthony Muchiri.

Famba anachukua wadhifa wa Simon Rotich ambaye muda wake wa kuhudumu umefikia mwisho. Aliteuliwa Agosti Mosi mwaka 2019.

Watu 11 waliteuliwa ili kusailiwa kwa wadhifa huo Mei 10, 2024 ambapo Famba aliibuka mshindi.

Wengine ni Brian Muithya Mutie, Judy Wangechi, Irene Cherotich Asienga, Sylvester Odhiambo Obong’o, Mahat Osman Shale, Joan Machayo, Christopher Leparan Tialal, Bahati Keranga Mwita, Gababo Dido Jillo na Juliana Nashipae Yiapan.

Usaili ulitekelezwa kwa siku mbili Mei 22 na 23, 2024.