Home Habari Kuu Pasipoti kuwa tayari ndani ya siku tatu pekee kuanzia Septemba asema Kindiki

Pasipoti kuwa tayari ndani ya siku tatu pekee kuanzia Septemba asema Kindiki

0
Waziri Kindiki akijaribu matambo mpya wa kuchapisha pasipoti katika jumba la Nyayo

Waziri wa usalama wa kitaifa Kithure Kindiki, amesema kuwa wale watakaotuma maombi ya pasipoti kuanzia Septemba mosi mwaka huu watazipata ndani ya muda wa siku tatu ,kutoka siku ya kutuma ombi.

Wazriri Kindiki amesema itachukua kipindi cha siku 21 kupokea pasipoti kuanzia Mei mosi mwaka huu,huku muda huo ukipunguzwa hadi siku tatu kufikia Septemba.

Kindiki amesema hali imeboreshwa kufuatia ununuzi wa mitambo mipya Jumatatu iliyopita.

Wakenya wamekuwa wakilalamikia ucheleweshwaji wa kupata pasipoti, huku wenye safari za ughaibuni za dharura wakiathirika pakubwa.

Imebainika kuwa takriban pasipoti 724,000 zilizokuwa hazijachapishwa kufikia tarehe 11 mwezi uliopita, imepunguzwa kwa kiwango kikubwa.

Kindiki ameongeza kuwa pasipoti 50,000 zimechapishwa ndani ya wiki moja iliyopita na ziko tayari kucukuliwa na waliotuma maombi.

Website | + posts