Home Kimataifa Pasipoti 110,059 hazijachukuliwa na wenyewe, imesema idara ya uhamiaji

Pasipoti 110,059 hazijachukuliwa na wenyewe, imesema idara ya uhamiaji

Ili kuhakikisha uchapishaji wa paspoti unaharakishwa, Bitok alisema serikali imewekeza kwenye idadi ya wafanyakazi na vifaa vya kisasa  miongoni mwa hatua nyingine.

0
Serikali yaimarisha utoaji wa Pasipoti.
kra

Idara ya uhamiaji imesema pasipoti 110,059 hazijachukuliwa na wenyewe katika afisi za idara hiyo kote nchini.

Kupitia mtandao wa X, katibu katika idara ya uhamiaji Julius Bitok, alidokeza kuwa ili kurahisisha utoaji wa hati za usafiri,  imesitisha masharti yanayowalazimu watu kusubiri kwa muda fulani ili kupata paspoti.

kra

Bitok alisema wizara hiyo itaondoa pasipoti ambazo bado hazijachukuliwa katika muda wa miezi sita.

Nairobi inaongoza kwa idadi ya hati hizo ambazo hazijachukuliwa ambazo ni 55,504, ikifuatwa na Kisumu 11,707, Embu 10,816, mombasa 8,696, Nakuru 8,615, Eldoret 8,551, Kisii 5,719, Kericho 389 na Bungoma 62.

Aidha katibu huyo alisema idara hiyo imeimarisha uchapishaji wa pasipoti kuhakikisha watu waliopata ajira ughaibuni wanapata hati hiyo haraka iwezekanavyo, kuambatana na agizo la Rais William Ruto.

Ili kuhakikisha uchapishaji wa paspoti unaharakishwa, Bitok alisema serikali imewekeza kwenye idadi ya wafanyakazi na vifaa vya kisasa, miongoni mwa hatua nyingine.

Hivi majuzi Rais William Ruto alitangaza kwamba, watu  ambao wamepata ajira katika nchi za kigeni watapata hati za usafiri katika muda wa wiki moja.

Bitok aliwataka wale wanaowasilisha maombi ya paspoti  kwa dharura, wawasilishe stakabadhi zao  kwa taasisi husika. Ili kupunguza mrundiko wa maombi ya paspoti.