Home Michezo Paris Olympics: Gathimba na Cherotich kujitosa uwanjani Alhamisi

Paris Olympics: Gathimba na Cherotich kujitosa uwanjani Alhamisi

0
kra

Samuel Gathimba Kireri atakuwa mwanariadha wa kwanza wa Kenya kujitosa uwanjani Alhamisi, Agosti 1, 2024 huku mchezo wa riadha ukianza ramsi katika mashindano ya Olimpiki jijini Paris, Ufaransa.

Gathimba aliye na umri wa miaka 36 anajivunia kutwaa ubingwa wa Afrika mara mbili na pia ni bingwa wa Jumuiya ya Madola.

kra

Atashiriki fainali ya matembezi kilomita 20 kuanzia saa mbili unusu ikiwa siku ya kwanza ya Riadha jijini Paris nchini Ufaransa.

Baadaye, saa sita mchana, itakuwa zamu ya Zeddy Cherotich kupambana na Patricia Sampaio wa Ureno katika kilo 78 raundi ya 32 mchezo wa Judo.

Cherotich ndiye mwanadada wa kwanza na mchezaji Judo pekee wa Kenya katika Olimpiki ya mwaka huu.

Hadi sasa, China ingali kuongoza jedwali la medali kwa nishani 19, dhahabu 9, fedha 7 na shaba 3 huku wenyeji Ufaransa wakiwa wa pili kwa dhahabu 8, fedha 10 na shaba 8.

Afrika Kusini ni ya kwanza Afrika ikiwa ya 16 kwa dhahabu 1 na shaba 2.

Makala ya 33 ya Olimpiki yanashirikisha wanamicehzo wapatao 10,000 kutoka mataifa zaidi ya 200 na  yatakamilika tarehe 11 mwezi huu.

Website | + posts