Home Kimataifa Paris Olympics: Faith Cherotich aponyoka na shaba ya mita 3,000 kuruka viunzi...

Paris Olympics: Faith Cherotich aponyoka na shaba ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji

0
kra

Faith Cherotich aliinyakulia Kenya nishani ya shaba katika fainali ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji Jumanne usiku katika Michezo ya Olimpiki jijini Paris, Ufaransa.

Cherotich ambaye ni mshindi wa medali ya shaba ya mashindano ya dunia mwaka uliopita, alimaliza wa tatu kwa dakika 8 sekunde 55.15, ambao ni muda wake bora wa binafsi.

kra

Mzawa wa Kenya Winfred Yavi Mutile raia wa Bahrain alishinda medali ya dhahabu, akiweka rekodi  mpya ya Olimpiki ya dakika 8 sekunde 52.76.

Bingwa wa Olimpiki wa mwaka 2021 mjini Tokyo Peruth Chemutai wa Uganda aliridhia nishani ya fedha.

Awali, Wakenya waliambulia patupu kwenye fainali ya mita 1,500 wanaume, Cole Hooker wa Marekani akishinda dhahabu kwa muda wa rekodi mpya ya Olimpiki wa dakika 3 sekunde 27.65.

Mwingereza Josh Kerr alinyakua nishani ya fedha huku shaba ikimwendea Yared Nuguse wa Marekani.

Wakenya Timothy Cheruiyo na Brian Komen walimaliza katika nafasi mbili za mwisho 11,12 mtawalia.

 

Website | + posts