Home Kimataifa Papa Francis hatahudhuria mkutano wa COP28

Papa Francis hatahudhuria mkutano wa COP28

Papa Francis amekuwa akikabiliwa na matatizo kadhaa ya kiafya mwaka huu.

0

Papa Francis ameahirisha safari yake ya mkutano wa COP28 wa hali ya hewa mjiniDubai kutokana na mafua na kuvimba kwa mapafu, Vatican ilisema.

Papa, 86, alitarajiwa kuanza ziara ya siku tatu siku ya Ijumaa.

Mapema siku ya Jumanne, Vatican ilikuwa imesema inapanga kuendelea na safari licha ya kuwa mgonjwa mwishoni mwa juma.

Papa alikuwa amekubali kutosafiri “kwa masikitiko makubwa” baada ya kuombwa asiende na madaktari wake, ilisema.

“Ingawa hali ya afya ya Papa kw aujumla imeimarika kuhusiana na mafua na kuvimba kwa njia ya upumuaji, madaktari wamemwomba papa asifanye safari iliyopangwa kwa siku zijazo huko Dubai,” Vatican ilisema.

Siku ya Jumamosi, Papa alighairi matukio kutokana na kile Vatican ilichoeleza kuwa “dalili za mafua mepesi”.

Alifanyiwa uchunguzi wa CT scan ambao ulinyesha hana homa ya mapafu lakini alipatikana na uvimbe.

Kwa ajili ya baraka zake za kila wiki na ujumbe wa Jumapili alionekana akiwa ameketi kwenye kanisa la makazi yake badala ya St Peter’s Square, huku msaidizi akisoma ujumbe wake na bendeji iliyoshikilia mirija ya mishipa ilionekana mkononi mwake.

Papa Francis amekuwa akikabiliwa na matatizo kadhaa ya kiafya mwaka huu.

Alilazwa hospitalini akiwa na ugonjwa wa mkamba mwezi Machi na alifanyiwa upasuaji wa tumbo kwenye ngiri mwezi Juni.

Website | + posts
BBC
+ posts