Home Habari Kuu Papa Francis aomba msamaha kwa madai ya kutumia lugha mbaya kwa mashoga

Papa Francis aomba msamaha kwa madai ya kutumia lugha mbaya kwa mashoga

0

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, ameomba msamaha kwa madai kuwa alitumia lugha mbaya kwa mashoga na tena kukanya kuwa wasiruhusiwe kuwa mapadri wakati wa kikao cha siri na askofu.

Taarifa hizi ziliibua shutuma nyingi duniani ikizingatiwa kuwa, Papa yuko kipaumbele katika kupigia debe ndoa za jinsia moja.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mamlaka inayosimamia kanisa Katoliki iliyoko nchini ltalia, Matteo Bruni, ” Papa anafahamu kuhusu taarifa iliyochapishwa wakati wa kikao chake na askofu”.

Aliongeza kuwa, “na jinsi ambavyo ameeleza mara kadhaa kanisani ni kuwa, kuna nafasi ya kila mmoja, jinsi tulivyo”.

Alimalizia kuwa, ” Papa anaomba msamaha kwani hakunuia kutumia lugha chafu na anaomba msamaha kwa mtu yeyote ambaye anahisi kudunishwa au kukwazika na maneno hayo”.

Vile vile, wafuasi wa Papa huyo kutoka nchini Uhispania walimtetea wakisema kuwa haifahamu lugha ya kitaliano Kwa undani na aitumiapo,mara kadhaa huwa na maana tofauti na ile aliyoikusudia.

Tukio hili linajiri wakati kungali na misimamo mseto katika kanisa hilo kuhusu amri ya Papa ya kuwataka mapadri kubariki ndoa ya jinsia moja.

Hapa nchini Kenya, swala la ndoa ya jinsia lilipingwa vikali na wananchi, serikali na viongozi wa tabaka mbalimbali.

Boniface Musotsi
+ posts