Home Michezo Osimhen na Oshoala waibuka kidedea tuzo za wanasoka Afrika

Osimhen na Oshoala waibuka kidedea tuzo za wanasoka Afrika

0

Mshambulizi wa Nigeria na Napoli Victor Osimhen na nyota Super wa Falcons na Barcelona Assisat Oshoala,ndio wanandinga bora Afrika mwaka 2023 kwenye tuzo zilizoandaliwa mjini Marrakech Morocco Jumatatu usiku.

Osimhen alifunga magoli 26 kuisaidia Napoli kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Italia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 33.

Osimhen aliwapiku Achraf Hakimi wa Morocco,na Mohamned Salah, aliyemaliza wa pili mwaka ulopita.

Osimhen ndiye mchezaji wa kwanza kunyakua tuzo hiyo kutoka Nigeria tangu Nwanko Kanu mwzka 1999.

Oshoala kwa upande wake alitawazwa mshindi kwa mara ya sita kwajumla akiwashinda Thembi Kgatlana wa Afrija Kusini na
Barbara Banda wa Zambia.

Wallid Regragui wa Morocco alitawazwa kicha bora kwa wanaume huku Yaccine Bono akinyakua tuzo ya kipa bora.

Halfa hiyo ilihudhuriwa na Rais wa CAF Dkt Patrice Motsepe.

Website | + posts