Home Biashara Oparanya asema mipango haramu ya uwekezaji inafilisisha Wakenya

Oparanya asema mipango haramu ya uwekezaji inafilisisha Wakenya

0
kra

Aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya ambaye amependekezwa kuwa Waziri wa Vyama vya Ushirika na Biashara Ndogo na za Kadri, amesema kwamba mipango haramu ya uwekezaji almaarufu “pyramid schemes” inafilisisha Wakenya.

Akizungumza katika majengo ya bunge wakati wa usaili wake, Oparanya alisema kwamba Wakenya wanafaa kufanya utafiti katika afisi za serikali kabla ya kuwekeza katika mpango usio rasmi nchini.

kra

Oparanya alisema pia kwamba Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC inafaa kutekeleza uchunguzi wa kina kuhusu ubadhirifu wa pesa katika Chama cha Kitaifa cha Vyama vya Akiba na Mikopo, KUSCCO.

Iwapo uteuzi wake utaidhinishwa na bunge, Oparanya alisema atalainisha masuala katika chama cha wakulima wa kahawa nchini na kampuni ya kutayarisha maziwa ya New KCC kwani wakulima wanapoteza pesa zao kutokana na usimamizi mbaya.

Gavana huyo wa zamani alitetea sekta ya vyama vya ushirika, akiba na mikopo akisema ni muhimu kwani kuna vyama elfu 30 vilivyosajiliwa ambavyo mali yao jumla ni bilioni 1.7 lakini ni elfu 10 tu ambavyo vinafanya kazi.

Vyama hivyo alisema vitafanikisha ukuaji wa biashara ndogo na za kadri ambazo zimetoa ajira kwa watu milioni 15. Aliahidi kuhakikisha wanabiashara hao wanahamasishwa kuhusu usimamizi wa mapato yao.

Kuhusu Hustler Fund, Oparanya alisema kwamba yeye ni mmoja wa waliopinga hazina hiyo lakini baada ya kupata maelezo, anahisi ni mpango mzuri.

Website | + posts