Bingwa wa Jumuiya ya madola katika mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala atajitosa ugani Stade De France, Jumapili usiku katika michezo ya Olimpiki jijini Paris,akilenga kuwa Mkenya wa kwanza kufuzu kwa fainali.
Miaka mitatu iliyopita Omanyala ambaye ndiye mwanariadha mwenye kasi barani Afrika katika mita 100 alibanduliwa katika hatua ya semi fainali .
Omanyala aliye na umri wa miaka 28 ataingia semi fainali, akiwa mwanariadha wa pili mwenye kasi akijivunia sekunde 9.79 mwaka huu.
Katika nusu fainali Mkenya huyo amejumuishwa katika mchujo wa tatu wa Jumapili pamoja Kishane Thompson wa Jamaica,Andre De Grasse wa Canada,Zharnel Hughes wa Uingereza na Fred Kerley wa Marekani.