Home Michezo Omanyala asajili ushindi wa kwanza wa Diamond League

Omanyala asajili ushindi wa kwanza wa Diamond League

Omanyala aliziparakasa mbio hizo kwa sekunde 9 nukta 92 akimshinda chipukizi wa Botswana Letsile Tebogo aliyemaliza wa pili kwa sekunde 9 nukta 93.

0
kra

Bingwa wa jumuiya ya madola Ferdinand Omanyala hatimaye aliandikisha historia kwa kushinda mbio za mita 100 katika mashindano ya Diamond League kwa mara ya kwanza Ijumaa usiku katika mkondo wa Monaco.

Omanyala aliziparakasa mbio hizo kwa sekunde 9 nukta 92 akimshinda chipukizi wa Botswana Letsile Tebogo aliyemaliza wa pili kwa sekunde 9 nukta 93.

kra

Omanyala ambaye pia ni bingwa wa Afrika alikuwa amemaliza wa pili katika mikondo ya Florence na Paris Diamond League akishindwa na bingwa wa dunia Fred Kerley wa Marekani.

Matokeo hayo yanamtia motisha Omanyala anapojiandaa kushiriki mashindano ya riadha duniani mwezi ujao mjini budapest Hungary akilenga kuweka historia kuwa mkenya wa kwanza kushinda dhahabu.

Omanyala alikosa kufuzu kwa fainali ya mashindano ya dunia aliposhiriki kwa mara ya kwanza mwaka uliopita alipolemewa katika hatua ya semi fainali.

Website | + posts