Home Kimataifa Omanyala afuzu kwa nusu fainali ya mita 100 Olimpiki

Omanyala afuzu kwa nusu fainali ya mita 100 Olimpiki

0
kra

Mshikilizi wa rekodi ya Afrika Ferdinand Omanyala amefuzu kwa nusu fainali ya mita 100 katika michezo ya olimpiki jijini Paris Ufaransa .

Omanyala ambaye pia ni bingwa wa Jumuiya ya madola  ameongoza mchujo pili siku ya Jumamosi akifyatuka kwa sekunde 10.08.

kra

Mkenya huyo atarejea kwa nusu fainali Jumapili usiku akiwa mchujo wa tatu pamoja na Kishane Thompson wa Jamaica, anayeorodheshwa wa kwanza kwa kasi,Zhanel Hughes wa Uingereza   na Fred Kerley wa Marekani miongoni mwa wapinzani wengine.

Omanyala atashiriki nusu fainali akilenga kufuzu kwa fainali ya Olimpiki kwa mafa ya kwanza baada ya kubanduliwa katika hatua hiyo, kwenye makala ya mwaka 2021 mjini Tokyo.

 

Website | + posts