Home Michezo Olunga kununua klabu ya Eskilstuna ya Uswidi

Olunga kununua klabu ya Eskilstuna ya Uswidi

0

Nahodha wa Harambee stars Micheal Olunga, yumo kwenye hatua za mwisho za mazungumzo ya kununua klabu ya FC Eskilstuna ya nchini Uswidi.

Mshambulizi huyo ambaye husakata soka ya kulipwa klabuni Al-Duhail nchini Qatar, amechangia pakubwa katika kukuza soka humu nchini kupitia wakfu wa Micheal Olunga Football Academy -MOFA.

Timu hiyo ambayo hushirki divisheni ya kwanza kanda B, inashirikiana na shule kadhaa  kama vile  Agoro Sare, Kisumu Day na St.Mary’s Yala Kwa lengo la kukuza vipaji vya soka nchini.

Hata hivyo, hatua ya umiliki upya wa klabu hiyo imetokana na masaibu chungu nzima inayopitia klabu hiyo.

Kwa sasa Eskilstuna imepigwa marufuku kutumia uwanja wa manispaa kwa sababu ya deni la shilingi milioni sita, na pia wanadaiwa shilingi milioni 41 walizopewa na wakala wa ukuzaji talanta.

MOFA iko tayari kulipa madeni hayo naye Olunga aongeze shilingi milioni 50, huku akijivunia kulipwa mshahara wa shilingi milioni 6 Kwa wiki.

Klabu hiyo ilipitia wakati mgumu uwanjani hasa msimu wa 2017, iliposhushwa ngazi licha ya mabadiliko ya uongozi na kulazimika kubadilisha jina kutoka Solna.

Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kuwa, mashabiki wa klabu wana furaha na imani kuwa, ujio wa Olunga utaimarisha klabu hiyo wakisubiria uamuzi wa mwisho.

Endapo Olunga atatwaa timu hiyo huenda ikawapa vijana wengi wa humu nchini kupiga soka ya kulipwa nchini humo.

Wakenya Henry Mejja na Frank Odhiambo wanaichezea  klabu hiyo.