Home Kimataifa Ogamba: WFP hufanikisha mpango wa lishe shuleni

Ogamba: WFP hufanikisha mpango wa lishe shuleni

0
kra

Waziri wa elimu Julius Ogamba, amesema mpango wa chakula dunia WFP, hutekeleza jukumu muhimu kushirikisha usaidizi kutoka kwa washirika kupiga jeki mpango wa serikali wa kutoa lishe shuleni.

Waziri huyo alisema kuwa WFP,  imefanikisha kuongeza idadi ya wanafunzi walio katika mpango huo kutoka Milioni 2.5 hadi Milioni 10 kwa siku.

kra

Aliyasema hayo leo Alhamisi alipokutana na ujumbe kutoka WFP, ukiongozwa na mwakilishi wake hapa nchini Lauren Landis afisini mwake.

Waziri Ogamba alidokeza kuwa mpango wa lishe shuleni unaotekelezwa na Mama Taifa Rachael Ruto, umesaidia pakubwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaonufaika na mpango huo.

Mwakilishi wa WFP hapa nchini Lauren Landis, alipongeza Waziri Ogamba kwa kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mawaziri wa elimu kote duniani wakati wa kongamano kuhusu lishe shuleni mwezi Oktoba, utakaoandaliwa hapa nchini.

Wengine waliokuwepo ni pamoja na Katibu wa elimu ya msingi Dkt. Belio Kipsang miongoni mwa wengine.

Website | + posts