Home Michezo Obiri akosa Jackpot ya Marathon baada ya kumaliza wa pili

Obiri akosa Jackpot ya Marathon baada ya kumaliza wa pili

0

Bingwa wa New York City Marathon mwaka 2023 Hellen Obiri alikosa Jackpot ya marathon mwaka huu, baada ya kumaliza wa pili nyuma ya Sifan Hassan wa Uholanzi.

Obiri aliyekuwa ameshinda mbio za Boston Marathaon mwaka huu akishiriki kwa mara ya kwanza, alimaliza katika nafasi ya kwanza kwa pointi 50 sawa na Sifan ambaye alishinda mbio za London Marathon na Chicago akiweka muda wa kasi wa saa 2, dakika 13 na sekunde 44.

Ilibidi wakurugenzi sita wa mbio kuu duniani za marathon wapige kura ili kubaini mshindi wa kitita cha dola 50,000 za Marekani sawa na shilingi milioni 7.5.

Sifan alishinda kura ya turufu na kutawazwa bingwa wa msimu akifuatwa na Obiri aliyezawadiwa dola 25,000.

Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya marathon kwa wanaume Kelvin Kiptum, alitwaa tuzo ya wanaume baada ya kushinda mbio za Boston na Chicago akizoa alama 50.

Website | + posts