Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria amefichua kuwa serikali inanuia kusajili vijana 30,000 kujiunga na huduma ya taifa kwa vijana, NYS mwaka huu.
Kuria amesema kuwa usajili wa kwanza utaandaliwa mwezi huu kwa vijana 10,000 huku ule wa pili ukiratibiwa kuandaliwa mwezi Julai mwaka huu pia ukilenga vijana 10,000.
Awali, Kuria alitoa agizo mwaka uliopita kutaka usajili wote wa makurutu wa vikosi vya polisi, jeshi na magereza kuwa na asilimia 30 ya vijana kutoka NYS.
Waziri amesisitiza kuwa vijana watakaohitimu pia watapewa kipaumbele kwa kazi za humu nchini na zile za ughaibuni.