Home Michezo Nyota wa Zambia Grace Chanda kukosa kombe la dunia

Nyota wa Zambia Grace Chanda kukosa kombe la dunia

Chanda alie na umri wa miaka 26 ameichezea timu hiyo almaarufu Copper Queens mechi 28 na amekuwa nguzo muhimu kwa kuifizisha kwa kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

0

Timu ya Zambia imepatwa na pigo katika harakati zake za kushiriki fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza, baada ya kiungo wao mshambuliaji Grace Chanda kujeruhiwa na atakosa fainali za mwaka huu.

Kulingana na matabibu wa timu Chanda alipata jeraha na hatapokana kwa wakati ufao huku likiwa pigo kubwa wa kwa timu hiyo inayoshiriki kombe la dunia kwa mara ya kwanza kabla ya mchuano wa ufunguzi kundini C dhidi ya Japan siku ya Jumamosi.

Mchezaji huyo ni majeruhi wa pili kwa Zambia baada ya kocha Bruce Mwape kulazimika kumwondoa kipa chaguo la kwanza Hazel Nali aliyepata jeraha la goti na nafasi yake kutwaluwa na chipukizi Leticia Lungu alie na umri wa miaka 18.

Chanda alie na umri wa miaka 26 ameichezea timu hiyo almaarufu Copper Queens mechi 28 na amekuwa nguzo muhimu kwa kuifizisha kwa kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here