Home Burudani Nyota wa Brooklyn Nine-Nine Andre Braugher afariki kufuatia saratani ya mapafu

Nyota wa Brooklyn Nine-Nine Andre Braugher afariki kufuatia saratani ya mapafu

0
kra

Muigizaji aliyeshinda tuzo ya Emmy mara mbili Andre Braugher alifariki kutokana na saratani ya mapafu baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa huo miezi kadhaa iliyopita, msemaji wake ameithibitishia BBC.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 61 alifariki siku ya Jumatatu.

kra

Braugher alijulikana sana kwa majukumu yake kama Kapteni Ray Holt katika kipindi chaBrooklyn Nine-Ninena Detective Frank Pembleton kwenye Homicide: Life on the Street.

Alishinda Emmy kwa uigizaji wakewaHomicide mnamo 1998 na lingine mnamo 2006 kwa kazi yake katika filamu ya ‘Thief’.