Home AFCON 2023 Nyangumi wa Cape Verde wafuzu raundi ya pili AFCON

Nyangumi wa Cape Verde wafuzu raundi ya pili AFCON

0

Timu ya taifa ya Cape Verde almaarufu Blue Sharks,  ndio timu ya kwanza kufuzu kwa raundi ya 16 bora katika kipute cha kwuania kombe la AFCON nchini Ivory Coast.

Nyangumi hao wamefuzu baada ya kuwang’ata nyoka ukipenda Mamba wa Msumbiji mabao matatu kwa bila katika mechi ya kundi B, iliyosakatwa Ijumaa jioni mjini Abidjan.

Bebe,Ryan Mendes na Kevin Leninin walifunga bao moja kila mmoja kwa Cape Verde wakisajili ushindi wa pili mtawalia baada ya kuilaza  Ghana 2-1 katika mechi ya ufunguzi.

Blue Sharks wanaongoza kundi B kwa alama 6, wakifuatwa na Misri kwa pointi 2 huku Ghana ikiwa na alama moja .

Ghana watakamilisha ratiba dhidi ya Msumbiji Jumatatu huku Misri wakimenyana na cape Verde.

 

Website | + posts