Home Kimataifa NTSA yakanusha kuwepo uhaba wa nambari za usajili wa magari

NTSA yakanusha kuwepo uhaba wa nambari za usajili wa magari

Mnamo tarehe 13 mwezi huu NTSA iliweka anwani ambapo wauzaji magari na waendeshaji wanaweza kupata nambari zao za usajili na leseni.

0

Halmashauri ya kitaifa ya uchukuzi na usalama barabarani (NTSA) imekanusha madai kwamba kuna uhaba wa nambari za usajili wa magari nchini.

Kwenye taarifa katika mtandao wa X, NTSA ilisema kuwa kuna zaidi ya nambari laki moja za usajili ambazo hazijachukuliwa katika afisi zake kote nchini.

Ilisema kuwa wauzaji magari na wamiliki wa magari kwa sasa wanachukua nambari zao za usajili kutoka kwa vituo walivyochagua walipowasilisha maombi yao.

Mnamo tarehe 13 mwezi huu NTSA iliweka anwani ambapo wauzaji magari na waendeshaji wanaweza kupata nambari zao za usajili na leseni.

NTSA ilisema kuwa watu hawahitaji kujisajili kwani hakuna malipo.

Ili kupata anwani hiyo mwasilishaji ombi anaweza kutumia nambari yake ya kitambulisho na kutumia nambari ya usajili ya gari au pikipiki kutafuta nambari za usajili.

Website | + posts