Home Habari Kuu NTSA: Watumiaji barabara watakiwa kuwa makini zaidi

NTSA: Watumiaji barabara watakiwa kuwa makini zaidi

Halmashauri hiyo ilielezea wasiwasi kuhusiana na baadhi ya madereva kuendesha magari katika barabara zilizofurika, huku akiwahimiza kusitisha hali hiyo.

0

Halmashauri ya kitaifa ya uchukuzi na usalama barabarani NTSA, imewatahadharisha watumizi wa barabara kuwa waangalifu, dhidi ya hatari zinazoweza tokea wakati huu wa msimu wa mvua.

Katika taarifa kwa ukurasa wa X, halmashauri hiyo iliwataka madereva kutoendesha magari kwa kasi, kwa kuwa sehemu za barabara kadhaa ni telezi, au zina mafuriko hali ambayo huenda ikasababisha ajali.

Halmashauri hiyo ilielezea wasiwasi kuhusiana na baadhi ya madereva kuendesha magari katika barabara zilizofurika, huku ikiwahimiza kusitisha hali hiyo.

Aidha abiria pia wametakiwa kuwajibikia usalama wao na kuwaripoti madereva wanaokiuka sheria za barabarani.

Halmashauri ya NTSA ilisema imejitolea kudumisha usalama barabarani na kutangaza kuwa ikishirikiana na maafisa wa polisi,  zitatekeleza utathmini wa kuzingatia kanuni za usalama barabarani katika barabara kuu za humu nchini.