Home Kimataifa NPS: Taarifa za usajili wa maafisa wapya wa polisi Januari ni za...

NPS: Taarifa za usajili wa maafisa wapya wa polisi Januari ni za uongo

0

Huduma ya Taifa ya Polisi, NPS imewataka Wakenya kupuuzilia mbali taarifa za kupotosha zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikiashiria kuwa zoezi la kuwasajili maafisa wapya wa kujiunga na huduma hiyo limepangwa kufanyika mwezi huu. 

Kwa mujibu wa NPS, taarifa hizo zilidai zoezi hilo limepangwa kufanyika Januari 5, 2024.

“Tungependa kuutarifu umma kupuuzilia mbali taarifa za uongo zinazoenea katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kusajiliwa kwa maafisa wa kujiunga na Huduma ya Taifa ya Polisi mwezi Januari, 2024,” ilisema NPS katika taarifa.

Taarifa za uongo juu kusajiliwa kwa maafisa wa polisi katika NPS hufungua milango ya matapeli kuwalaghai watu wasiokuwa na habari maelfu ya pesa kwa ahadi kuwa watawasaidia kujiunga na huduma hiyo.

Ukosefu wa ajira ni suala sugu nchini Kenya na wengi hujipata wakinaswa na mtego wa walaghai hao wakati wakitumai kujipatia ajira iliyowakwepa kwa muda mrefu na hivyo kupiga dafrau gaharama ya juu ya maisha inayowaelemea.

Website | + posts