Home Kimataifa Norway kufunga ubalozi wake nchini Uganda

Norway kufunga ubalozi wake nchini Uganda

0
Balozi wa Norway nchini Uganda na Rais Museveni

[contact-form][contact-field label=”Name” type=”name” required=”true” /][contact-field label=”Email” type=”email” required=”true” /][contact-field label=”Website” type=”url” /][contact-field label=”Message” type=”textarea” /][/contact-form]

[contact-form][contact-field label=”Name” type=”name” required=”true” /][contact-field label=”Email” type=”email” required=”true” /][contact-field label=”Website” type=”url” /][contact-field label=”Message” type=”textarea” /][/contact-form]

Taifa la Ulaya kaskazini la Norway limetangaza kwamba litafunga ubalozi wake jijini Kampala nchini Uganda mwakani.

Kupitia taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Norway nchini Uganda Ijumaa, nchi hiyo imeelezea kwamba hatua hiyo ni sehemu ya mabadiliko ambayo inatekeleza katika mipango yake ya mambo ya nje.

Taarifa hiyo ilisema kwamba mabadiliko mengi yanatarajiwa katika uwepo wa Norway kidiplomasia ughaibuni, kwa nia ya kuhudumia vyema maslahi ya nchi hiyo.

Julai mwaka jana Norway ilifunga balozi ndogo 5 na sasa ni zamu ya ubalozi wa Uganda ambao utafungwa rasmi Julai 2024.

Norway imekuwa na ubalozi wake jijini Kampala nchini Uganda tangu mwaka 1994 na umekuwa pia ukishughulikia mahusiano yake na nchi za Rwanda and Burundi.

Taarifa hiyo ilifafanua kwamba ushirikiano wa kimaendeleo na Uganda hautaathiriwa na hatua ya kunga ubalozi kwani uhusiano kati ya nchi hizo mbili utaendelea kuwepo.

Shirika la Norad litajukumiwa kusimamia ushirikiano wa aina yoyote na Uganda siku za usoni likisaidiwa na ubalozi wake katika nchi moja ya kanda hii ambayo haikutajwa.

Norway husaidia katika miradi kadhaa nchini Uganda ikiwa ni pamoja na sekta ya elimu, afya, kilimo na hata usaidizi wa wakimbizi.

Website | + posts