Home Kimataifa Njuri Ncheke: Waziri Kindiki ndiye kiongozi wa Mlima Kenya

Njuri Ncheke: Waziri Kindiki ndiye kiongozi wa Mlima Kenya

0
Waziri wa usalama wa taifa Prof. Kithure kindiki.
kra

Zaidi ya wazee 2,000 wa Njuri Ncheke kutoka Meru na Tharaka Nithi, wamemuidhinisha waziri wa usalama wa taifa Prof. Kithure Kindiki, kuwa kiongozi mpya wa eneo la mlima Kenya.

Wakizungumza leo Jumatano katika madhabahu ya Ncheru, Tigania Magharibi kaunti ya Meru, wazee hao walitangaza kujitenga na naibu Rais Rigathi Gachagua, wakielezea imani yao kwa waziri Kindiki, ambaye atakuwa kiunganishi kati yao na Rais William Ruto.

kra

Wakiongozwa na mwenyekiti mpya wa kaunti ya Meru Adrian Aruyaru, wazee hao kutoka kaunti za Meru na Tharaka Nithi, walisema waziri Kindiki ameshirikiana kwa karibu na Rais William Ruto.

Aidha wazee hao walielezea kumuunga mkono Gavana wa Meru Kawira Mwangaza, wakidokeza kuwa wanatambua serikali ya kaunti iliyoko mamlakani.

Waliwahimiza Gavana Mwangaza na mwenzake wa Tharaka Nithi  Muthomi Njuki, kushirikiana kwa karibu na Rais William Ruto, kwa maendeleo ya eneo hilo.

Wakati huo huo, walitoa wito wa umoja kati ya eneo la Mlima Kenya Mashariki na ile ya Magharibi, ili kufanikisha maendeleo katika maeneo hayo.

Website | + posts