Home Michezo Ni kufa kupona kwa Harambee Stars leo usiku

Ni kufa kupona kwa Harambee Stars leo usiku

0

Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars itashuka ugani Félix Houphouët Boigny mjini Abidjan nchini Ivory Coast leo Jumatatu usiku, kwa mchuano wa pili wa kundi F dhidi ya Ushelisheli kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026.

Mchuano huo utakuwa wa pili kwa Kenya waliopoteza mabao 2-1 dhidi ya Gabon wiki iliyopita.

Utang’oa nanga saa nne usiku kwa saa za Kenya.

Gabon wanaongoza kundi hilo kwa alama 6 baada ya kuishinda Burundi magoli mawili kwa moja jana Jumapili katika kiwara cha Benjamin Mkapa jijini Daresalaam.