Home Habari Kuu Ni afueni kwa wanafunzi baada yalishe shuleni kurejeshwa

Ni afueni kwa wanafunzi baada yalishe shuleni kurejeshwa

0

Watoto kutoka familia maskini nchini wana kila sababu ya kutabasamu, baada ya kamati ya elimu ya bunge la kitaifa  kurejesha mpango wa lishe shuleni wa  shilingi billioni 2 ambao ulikuwa umefutiliwa mbali na wizara ya fedha.

Mwenyekiti wa kamati hiyo,Julius Melly, alielezea kamati ya bunge ya makadario ya bajeti kuwa mpango huo ulirejeshwa kupitia bajeti ya baraza la Kitaifa la jamii za kuhamahama-NACONEK.

Kufuatia hatua hiyo mwenyekiti wa kamati ya makadirio ya bajeti  Ndindi Nyoro, alitaka kujua jinsi serikali itakavyomudu mpango huo ikitiliwa maanani kuwa hakuna bajeti ya ziada.

Mpango huo wa chakula umewafanya wanafunzi wengi kutoka familia zisizojiweza na hasa za mitaa yaduni  na zile za kuhamahama kuhudhuria masomo vyema.

Nyoro pia ameunga mapendekezo ya kamati ya elimu ya kuwaajiri walimu 46,000 wa sekondari  ya msingi (JSS), Kwa mkataba wa kudumu kutoka januari mwakani.

Kauli hiyo pia iliungwa mkono  na mjumbe wa Embakasi Mashariki Babu Owino.

Naye mbunge wa Samburu Magharibi Naisula Lesuuda amehimiza tume ya kuajiri walimu nchini TSC, kuwaajiri wanagenzi hao wa JSS ili watoe nafasi kwa wanagenzi wengine.

Boniface Musotsi
+ posts