Home Habari Kuu Umeme warejeshwa eneo la Mlima Kenya

Umeme warejeshwa eneo la Mlima Kenya

Nguvu za umeme zimerejeshwa katika uwanja wa ndege wa JKIA.

0

Kampuni ya Kenya Power imerejesha umeme Katika eneo la Mlima Kenya kufuatia kupotea kwa umeme katika maeneo mengi ya nchi Ijumaa usiku.

Kulingana na taarifa kutoka kwa kampuni ya KPLC, ukosefu huo wa umeme uliotokea Ijumaa saa tatu na dakika 45 usiku, ulisababishwa na hitilafu katika moja ya mitambo yake.

“Tunafanya kila juhudi kurejesha hali ya kawaida haraka iwezekanavyo,” ilisema taarifa ya KPLC.

Kufuatia kupotea kwa  umeme na kuathiri shughuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA),  Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen aliomba msamaha, akisema hakuna sababu ya ukosefu wa umeme katika uwanja huo wa ndege.

Halmashauri ya kusimamia viwanja vya ndege (KAA), ilisema jenereta ilikosa kuwaka na kusababisha ukosefu wa umeme.

Hata hivyo, umeme umerejeshwa katika uwanja wa ndege wa JKIA.

Website | + posts