Home Burudani Nguo ya Princess Diana yauzwa mnadani kwa pauni 900,000

Nguo ya Princess Diana yauzwa mnadani kwa pauni 900,000

0
Diana alivaa nguo ya Azagury kwa mara ya kwanza kwenye dhifa ya chakula cha jioni na Meya wa Florence mnamo 1985.

Nguo iliyovaliwa na Diana, Bintimfalme wa Wales mnamo 1985 imeuzwa kwenye mnada kwa bei iliyokadiriwa kuwa mara 11 zaidi ya bei halisi.

Gauni hilo la velvet nyeusi, ya urefu wa ballerina iliuzwa katika mnada wa Julien’s Auctions mjini Hollywood kwa kima cha dola 1,148,080

Imevunja rekodi mpya ya mitindo kwani nguo ya bei ghali zaidi, iliyovaliwa na Diana, kuuzwa kwenye mnada.

Gauni hilo, ambalo lilikuja na kielelezo kinacholingana, lilikadiriwa kuuzwa kwa dola 100,000 (£78,776).

Diana alivaa vazi hilo kwa mara ya kwanza mjini Florence, Italia mnamo 1985 kwenye dhifa ya chakula cha jioni akiwa kwenye ziara ya kifalme na mume wake wa wakati huo Mwanamfalme Charles, Mtawala wa Wales, na tena kwenye Orchestra ya Vancouver Symphony mnamo 1986.

Mavazi ya jioni ya Princess Dana ni mojawapo ya bidhaa nyingi za watu mashuhuri zinazouzwa katika minada ya Julien huko California.
BBC
+ posts