Home Biashara Ndege za abiria za KQ kuendelea kutua Tanzania

Ndege za abiria za KQ kuendelea kutua Tanzania

0

Mamlaka ya usafiri wa angani nchini Tanzania, TCAA imetangaza kwamba imeruhusu tena ndege za abiria za shirika la Kenya Airways, KQ kuendelea kuhudumu kati ya Nairobi na Dar es Salaam.

Mamlaka hiyo imetengua uamuzi wake wa jana ambapo ilitangaza kwamba imefutilia mbali vibali vya kampuni ya Kenya Airways kulingana na kanuni nambari tatu na nne za uhuru wa haki za trafiki.

TCAA ilisema uamuzi wa jana ulichochewa na hatua ya Kenya kukataa kukubalia ndege za mizigo za Air Tanzania kuhudumu kati ya Nairobi na nchi nyingine.

Sasa mkurugenzi mkuu wa TCAA, Hamza Johari ameelezea kwamba wamebatilisha uamuzi wa awali baada ya Kenya kukubali ombi la Tanzania kwamba Kenya iwe ikisafirisha mizigo yake yote kwa kutumia Kampuni ya Air Tanzania kuanzia leo Januari 16, 2024.

Haya ni kulingana na kwa kuzingatia sera nambari tano ya haki za trafiki.