Home Kimataifa Ndege ya Kenya Airways yatua kwa dharura

Ndege ya Kenya Airways yatua kwa dharura

Wahudumu wa afya waliofika kumpokea mgonjwa huyo, walimpeleka hospitalini kwa matibabu zaidi.

0
Ndege ya shirika la Kenya Airways.
kra

Ndege moja ya shirika la ndege la Kenya Airways, KQ iliyokuwa ikielekea Uingereza kutoka jijini Nairobi, ilitua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow baada ya abiria kuwa mgonjwa akiwa safarini.

Kupitia kwa taarifa, KQ ilisema abiria aliyekuwa ndani ya ndege ya KQ100 aliyekuwa akisafiri kutoka Nairobi kuelekea Heathrow, aligonjeka saa 14:19, na kusababisha ndege hiyo kutua kwa dharura siku ya Jumatatu.

kra

Kulingana na shirika hilo, kisa hicho kilitangazwa kuwa cha dharura na rubani kwa kitengo cha kudhibiti safari za ndege, ili kiharakishe kutua kwa ndege hiyo kutoa fursa kwa mgonjwa huyo kupata huduma za matibabu.

Aidha shirika hilo lilisema madaktari wawili na muuguzi mmoja waliokuwa ndani ya ndege hiyo, walimhudumia mgonjwa huyo.

Wahudumu wa afya waliofika kumpokea mgonjwa huyo, walimpeleka hospitalini kwa matibabu zaidi.

Website | + posts