Home Kimataifa Ndege ndogo yatua kwa dharura na kugonga jengo Paris

Ndege ndogo yatua kwa dharura na kugonga jengo Paris

0

Ndege ndogo ya injini mbili imelazimika kutua kwa dharura katika kitongoji cha kusini mwa Paris.

Watu watatu waliokuwemo ndani ya ndege hiyo walipelekwa hospitalini kuhitaji uangalizi wa haraka, lakini majeraha yao hayakuchukuliwa kuwa ya kutishia maisha, maafisa walisema.

Hakuna mtu mwingine aliyejeruhiwa katika tukio hilo. Ndege hiyo ilitua katika eneo la makazi huko Villejuif baada ya injini kuharibika, kulingana na Waziri wa Uchukuzi wa Ufaransa, Clément Beaune.

Watu watatu waliokuwemo ndani ya ndege hiyo walikuwa mwalimu wa safari za ndege mwenye umri wa miaka 80 na abiria wawili walio na umri wa miaka 20 hivi, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani.

Ndege hiyo ilianza kutua kwa dharura kwenye barabara kabla ya kugonga ukuta wa jengo la ghorofa.

Hatimaye ilisimama kwenye bustani iliyokuwa nyuma ya jengo la ghorofa, huku sehemu za ndege zikiwa zimetapakaa juu ya paa la karakana iliyokuwa karibu.

Mkia wa ndege ulitenganishwa na sehemu nyingine ya ndege na mabawa yalivunjika kwa kiasi kikubwa.

BBC
+ posts