Home Kimataifa Ndege aina ya Boeing 737 yaanguka nchini Senegal

Ndege aina ya Boeing 737 yaanguka nchini Senegal

Rubani alijeruhiwa kidogo, lakini idadi kubwa ya abiria 78 waliokuwemo hawakujeruhiwa katika tukio hilo.

0
Ndenge aina ya 737 yaanguka nchini Senegal. Picha/Hisani.
kiico

Ndege aina ya Boeing 737-300 imeanguka wakati ikipaa nchini Senegal na kujeruhi watu 11, wanne kati yao vibaya.

Ndege ya Air Senegal HC 301 iliyokuwa ikielekea mji mkuu wa Mali Bamako ilitoka kwenye njia ya kurukia ndege mapema Alhamisi, Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Dakar wa Blaise Diagne ulisema katika taarifa.

Rubani alijeruhiwa kidogo, lakini idadi kubwa ya abiria 78 waliokuwemo hawakujeruhiwa katika tukio hilo.

Shughuli zimesitishwa katika uwanja wa ndege.

Huduma za dharura katika uwanja wa ndege zimasaidia kuwaondoa abiria, taarifa ya uwanja huo wa ndege ilisema.

Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha ajali.

Boeing haijazungumzia tukio hilo wala Transair, kampuni ya kibinafsi ambayo Air Senegal ilikodisha ndege hiyo

Ingawa bado haijajulikana ni nini kilisababisha ajali hiyo, inakuja wakati shirika la Boeing anakabiliwa na changamoto kubwa kuhusu usalama wa ndege zake.

kiico