Home Habari Kuu NCPB yawafidia wakulima waliouziwa mbolea bandia ya bei nafuu

NCPB yawafidia wakulima waliouziwa mbolea bandia ya bei nafuu

Kulingana na Kimote, NCPB hadi kufikia sasa imesambaza magunia milioni tatu ya mbolea ya gharama nafuu kwa wakulima wakati huu wa msimu wa mvua.

0
Mbolea ya gharama nafuu.

Halmashauri ya nafaka na mazo nchini NCPB, imanza zoezi la kuwafidia wakulima walionunua mbolea bandia ya gharama nafuu.

Mkurugenzi Mkuu wa NCPB Joseph Kimote, amesema hatua hiyo inafuatia agizo kutoka kwa wizara ya kilimo, kuwa wakulima wote walionunua mbolea hiyo kutoka kwa kampuni ya utengenezaji mbolea ya KEL, walipwe fidia.

“Wakulima wote walioathiriwa wanashauriwa kutuma malalmishi yao, ambayo yatawasilishwa katika kituo kilichowauzia mbolea hiyo. Wanapaswa kuwa na kitambulisho cha taifa, ushahidi kuwa walinunua mbolea hiyo,” alisema kimote.

Kimote alidokeza kuwa wakulima ambao tayari wametumia mbolea hiyo na NCPB imethibitisha kuwa waliinunua mbolea kutoka kwa maghala yake, watafidiwa na mbolea ya kiwango sawa na hicho ya upanzi.

“Ikiwa mkulima hakutumia mbolea hiyo, atahitajika kuirejesha katika ghala la NCPB na kisha kupatiwa mbolea ya upanzi ya kiwango sawa na alichonunua awali,” aliongeza Kimote.

Kulingana na Kimote, NCPB hadi kufikia sasa imesambaza magunia milioni tatu ya mbolea ya gharama nafuu kwa wakulima wakati huu wa msimu wa mvua.

Website | + posts