Home Biashara NCBA: Uchumi wa Kenya kukua hadi asilimia 6 2024

NCBA: Uchumi wa Kenya kukua hadi asilimia 6 2024

0
Mkurugenzi Mkuu wa NCBA Bank Group, John Gachora

Kongamano la Kiuchumi la NCBA limetabiri kuwa uchumi wa Kenya utakua hadi asilimia 6 mwaka 2024.

Ukuaji huo utatokana na kufufuka kwa sekta ya kilimo, uthabiti wa sekta ya utoaji huduma na hatua za serikali zinazolenga kuchechemua ukuaji katika sekta muhimu za uchumi ikiwa ni pamoja na kilimo na sekta za utengenezaji bidhaa.

Hata hivyo, NCBA inaonya kuwa gharama ya juu ya maisha isiyowahi kutokea inayosababisha athari hasi kwa mapato ya familia itaendelea kuwasababishia watu zaidi changamoto za kiuchumi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtazamo wa kiuchumi wa NCBA, Mkurugenzi Mkuu  wa NCBABank Group John Gachora alisema licha ya changamoto inayoshuhudiwa ya gharama ya juu ya maisha, hatua madhubuti zinaendelea kupigwa akiongeza kuwa serikali imeendelea kufanya marekebisho stahiki yatakayojitajika kuhakikisha uthabiti mkubwa wa kiuchumi.

Website | + posts