Home Kimataifa Navalny ahukumiwa miaka 19 gerezani

Navalny ahukumiwa miaka 19 gerezani

0

Mkosoaji mkuu wa serikali ya Urusi hasa kuhusu uvamizi wake nchini Ukraine Alexei Navalny amehukumiwa kifungo cha miaka 19 gerezani na mahakama moja ya Urusi kwa kile kinachotajwa kuwa makosa ya misimamo na itikadi kali.

Navalny ambaye ni wa upande wa upinzani nchini Urusi tayari anahudumia kifungo kingine cha miaka 9 katika gereza lililo na ulinzi mkali kwa makosa ya ulaghai na kudharau mahakama.

Mwezi Juni mwaka huu, alilaumiwa tena kwa kuunda kundi lenye itikadi kali, kufadhili mipango ya makundi kama hayo na kutengeneza kundi ambalo linakiuka haki za wananchi.

Navalny, aliyekamatwa mwaka 2021 na kuhukumiwa mwaka jana, alipata umaarufu ulimwenguni kwa kukashifu hatua ya Rais wa Urusi Vladimir Putin ya kuanzisha vita visivyo na maana yoyote nchini Ukraine. Amefichua pia habari za kibinafsi na mbaya kuhusu wafanyakazi wa serikali ya Putin.

Waendesha mashtaka katika kesi ya Navalny iliyoanza mwezi Juni, walikuwa wanataka ahukumiwe kifungo cha miaka 20 gerezani kwa makosa sita ya jinai yakiwemo makosa ya kuunda kundi la itikadi kali na kufadhili mipango ya makundi ya itikadi kali.

Navalny amekuwa akizuiliwa tangu mwaka 2021 baada ya kukiuka masharti ya msamaha wake baada ya kurejea nchini Urusi kutoka Ujerumani ambako alikuwa anatibiwa baada ya kutiliwa sumu na watu kutoka serikalini, jambo ambalo serikali ilikanusha.

Mwezi Machi mwaka huu, Navalny na wakfu wake wa kupambana na ufisadi walipatikana na hatia ya matumizi mabaya ya pesa walizokuwa wamepokea kama michango.

Hata baada ya hukumu hiyo ya kwanza, Navalny amekuwa akiendeleza ukosoaji wa serikali ya Urusi kupitia akaunti maarufu ya YouTube. Serikali imekua ikimtaka afunge akaunti hiyo lakini bado ipo.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here