Home Biashara Nauli ya matatu kuongezeka kwa asilimia 30 kuanzia Jumatano

Nauli ya matatu kuongezeka kwa asilimia 30 kuanzia Jumatano

0

Chama cha Wamiliki wa Matatu, MOA kimetangaza nyongeza ya nauli za matatu kwa asilimia 30 kuanzia kesho Jumatano.

Akiwahutubia wanahabari, mwenyekiti wa chama hicho Albert Karakacha, alisema hatua hiyo imeafikiwa kutokana na nyongeza ya ushuru wa bidhaa za mafuta kutoka asilimia 8 hadi 16.

“Nyongeza ya bei ya mafuta, ongezeko la gharama ya operesheni, riba za juu pamoja na bei ghali ya vifaa vya magari, ni chanzo cha nyongeza hiyo ya nauli ili kutuwezesha kuendelea kutoa huduma,” alisema Karakacha.

Wamiliki hao walielezea changamoto wamekuwa wakikumbana nazo hasa shinikizo za kifedha kutokana na nyongeza ya bei za mafuta, ambayo imetishia kusambaratisha biashara yao.

“Baada ya mashauriano na wadau, MOA kimeazimia kuongeza nauli ili kukabiliana na changamoto zilizopo. Kuanzia tarehe tano mwezi Julai, wasafiri watashuhudia nyongeza ya nauli ya kati ya asilimia 10 hadi 20,” aliongeza mwenyekiti huyo.

Hata hivyo, chama hicho kilisema kinatumia mbinu zote kukabiliana na athari za nyongeza hiyo, huku kikitoa wito kwa serikali kuweka ruzuku kwa bei za mafuta ili kuwapunguzia mzigo wahudumu wa matatu na abiria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here