Mwanamitindo maarufu duniani Naomi Campbell amekuwa mama kwa mara ya pili, akiwa na umri wa miaka 53.
Nyota huyo ambaye alimkaribisha mtoto wake wa kwanza miaka miwili iliyopita, alitangaza kuwasili kwa mtoto wake mtandaoni siku ya Alhamisi, na kuwaambia wafuasi wake “hatujachelewa”.
Hakuwa ameweka wazi kama anatarajia kupata mtoto wa pili na hakutoa maelezo zaidi kuhusu kuzaliwa kwake.
Mwanamitindo huyo wa Uingereza alisema kupita Instagram kuwa hii ni “zawadi ya kweli kutoka kwa Mungu”.
“Zawadi ya Kweli kutoka kwa Mungu, barikiwa! Karibu Babyboy. #mumoftwo.”
Campbell aliwahi kupamba vichwa vya habari kama hivyo mwaka 2021 alipotangaza kuwasili kwa mtoto wake wa kwanza wa kike kupitia Instagram.