Home Kimataifa Namibia kuchinja wanyapori zaidi ya 700 kuwalisha raia kutokana na makali ya...

Namibia kuchinja wanyapori zaidi ya 700 kuwalisha raia kutokana na makali ya njaa

0
kra

Namibia inapanga kuwachinja wanayamapori 723 wakiwemo tembo 83 na kusambaza nyama kwa raia ili kuwakimu kutokana na makali ya njaa.

kulingana na wizara ya mazingira nchini humo wanyama hao watachinjwa ndani ya mbuga zilizo na idadi kubwa kuliko eneo la malisho na maji ya kunywa yanayopatikana.

kra

Taifa hilo la Kusini mwa Afrika linakumbwa na kiangazi kibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa, huku nchini hiyo ikiwa imetumia zaidi ya asilimia 84 ya hifadhi ya chakula kulingana na Umoja wa Mataifa.

Zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini Namibia wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

Namibia inapanga kuchinjwa viboko 30,nyati 60,swara 50,kongoni 100,na pundamilia 300.

Website | + posts