Home Habari Kuu Nakhumicha: Serikali inashughulikia maswala ya Madaktari

Nakhumicha: Serikali inashughulikia maswala ya Madaktari

0

Waziri wa afya  Susan Nakhumicha ameelezea matumaini kuwa utata ulioko baina ya madaktari wanaogoma na serikali utasuluhishwa kufikia siku ya Jumatatu.

Akiwahutubia wananchi wakati wa ziara katika hospitali ya kaunti ndogo ya  Butere, hospitali ya Manyala na shule ya msingi ya  Esiatsala katika kaunti ya Kakamega, Nakhumicha ambaye aliandamana na naibu gavana wa kaunti ya Kakamega  Ayub Savula alisema serikali imejitolea kutafuta suluhu la kudumu kwa migomo ya mara kwa mara ya wahudumu wa afya.

Savula, mbunge wa  Butere  Tindi Mwale na mwakilishi wa kike katika kaunti ya Kakamega Elsie Muhanda walipuuzilia mbali hoja inayopangwa kuwasilishwa bungeni na mbunge wa Embakasi  Babu Owino ya kutokuwa na imani katika waziri wa afya kuhusiana na namna alivyoshughulikia mgomo wa madaktari.

Madaktari hao wanashinikiza maswala kadhaa kutekelezwa ikiwemo utekelezaji wa mkataba wa pamoja wa makubaliano uliotiwa saini na wizara ya fedha na kuajiriwa kwa madatari wanagenzi kwa masharti ya kudumu

Radio Taifa
+ posts