Home Habari Kuu Nakhumicha asisitiza umuhimu wa Afrika kuwekeza katika uundaji wa chanjo

Nakhumicha asisitiza umuhimu wa Afrika kuwekeza katika uundaji wa chanjo

0

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha Wafula amesisitiza umuhimu wa mataifa ya Bara Afrika kuwekeza katika utayarishaji wa dawa.

Alisema hayo kwenye kikao cha siku tatu kinachoendelea jijini Nairobi kuhusu upatikanaji wa chanjo barani Afrika.

Kikao hicho kinachohudhuriwa na wawakilishi wa mataifa mbali mbali ya Afrika ni jukwaa la kujadili kuhusu hatari inayokumba Afrika magonjwa yanapozuka na utegemezi katika uagizaji wa dawa kutoka ng’ambo.

Nakumicha aliangazia umuhimu wa kuziba pengo hilo haraka akipendekeza kuharakishwa kwa mipango ya kujitengeneza dawa.

Kulingana naye hatua hiyo ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa Afrika kukabiliana na dharura zozote za kiafya, kutoa nafasi za ajira na kuhimiza uvumbuzi ndani ya bara hili.

Kikao hicho kinalenga kuweka mikakati ya kuimarisha utengenezaji wa chanjo na mifumo ya upatikanaji wa dawa hizo barani Afrika lengo la msingi likiwa kuunda namna ya kuhakikisha uendelevu wa mifumo hiyo.

Mipango kama hiyo ni muhimu katika kuboresha jinsi ya kushughulikia mikurupuko ya magonjwa na upatikanaji sawa na wa haraka wa chanjo kwa wanaoathirika na magonjwa.

Kikao hicho kimeanza leo Januari 31 na kitaendelea hadi Februari 2, 2024 katika hoteli ya Mรถvenpick jijini Nairobi.

Kinawaleta pamoja watengenezaji wa chanjo wa Afrika, wanaotoa nyenzo na wadau wengine.

Website | + posts