Home Kaunti Naibu Chifu wa Siaya ajeruhiwa mazishini

Naibu Chifu wa Siaya ajeruhiwa mazishini

0
kra

Naibu Chifu wa kaunti ndogo ya Alego Usoga katika kaunti ya Siaya anauguza majeraha mabaya hospitalini baada ya kushambuliwa na kundi la vijana alipoamuru muziki unaofahamika sana kama “disco matanga” kutochezwa. 

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, naibu huyo alisikia sauti kubwa ya muziki katika eneo lake la utawala kisha akaanza kuchunguza chanzo chake.

kra

Alipobaina na kujaribu kuamuru usichezwe, vijana venye hasira walimshambulia kwa panga na vifaa butu na kumjeruhi vibaya, hali iliyowalazimu waombolezaji kumnusuru. Alikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya kaunti hiyo baada ya kujeruhiwa.

Kufuatia hali hiyo, askari wa kawaida na wa upelelezi walifika hospitalini humo na kuhakikisha kuwa alijeruhiwa kichwani na hali yake ilikuwa imedhoofika.

Baadaye, walianzisha msako mkali uliosababisha kutiwa nguvuni kwa mwanamume mshukiwa wa umri wa miaka 28 kwa jina Stephen Onyango.

Askari pia walipata vifaa butu vinavyoshukiwa kutumika katika kisa hicho huku mshukiwa huyo akifikishwa mahakamani.