Home Habari Kuu Naibu Rais Rigathi Gachagua kuhudhuria kongamano kuhusu chakula huko Italia

Naibu Rais Rigathi Gachagua kuhudhuria kongamano kuhusu chakula huko Italia

0

Naibu Rais Rigathi Gachagua aliondoka nchini Jumamosi kuelekea Italia kwa kongamano la siku tatu la shirika la umoja wa mataifa kuhusu kukadiria mifumo ya chakula litakaloanza Jumatatu jijini Roma.

Gachagua atahutubia kongamano hilo kwa niaba ya rais William Ruto aliyealikwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres.

Kwenye hotuba yake Naibu Rais ataangazia ufadhili wa mifumo ya chakula hasa mabadiliko kwenye mfumo wa chakula nchini Kenya, kama njia ya kutathmini kujitolea kwa nchi, serikali na wadau wengine katika kuwekeza fedha ilikumaliza njaa na utapiamlo.

Hotuba hiyo ya Gachagua itaandaa awamu ya viongozi wa serikali itakayohudhuriwa na waziri mkuu wa Italia Georgia Meloni na Guterres, kuzungumzia suala muhimu la uwepo wa chakula nyakati zote.

Lishe shuleni pia itazungumziwa kwenye mkutano huo ambapo nchi zitashirikiana na wadau wengine kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi wanapata chakula na katika kiwango faafu ili koboresha afya na elimu.

Katika kikao kingine ambacho kitahudhuriwa na viongozi wa nchi mbali mbali na wawakilishi wa mashirika ya umoja wa mataifa kuhusu chakula, Naibu Rais atazungumza kuhusu hatua ambazo Kenya imepiga tangu mwaka 1980, wakati mpango wa lishe shuleni ulianzishwa.

Mpango huo kwa sasa unafaidi wanafunzi milioni 1.6 hasa katika maeneo kame nchini na umesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaohudhuria masomo. Umesaidia pia kuhakikisha lishe bora kwa watoto hasa kupitia kwa maziwa.

Mwaka huu, serikali kwenye bajeti, iliongeza fedha za kufadhili mpango huo maradufu.

Balozi wa Kenya huko Italia Jackline Nyong’a anasema ni muhimu kwa Kenya kuhusika kwenye kongamano hilo wakati ambapo serikali inatekeleza mipango kadhaa ya kuboresha upatikanaji wa chakula ikitilia maanani mihemko ya mabadiliko ya tabianchi.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here