Home Biashara Naibu Rais Rigathi Gachagua akutana na wakurugenzi wa KTDA

Naibu Rais Rigathi Gachagua akutana na wakurugenzi wa KTDA

Wakulima wa majani chai mwaka huu wanatarajia kupata marupurupu yaliyoimarika, kufuatia mageuzi yaliyofanyiwa sekta hiyo ndogo, yaliyoshinikizwa na naibu huyo wa rais.

0
Naibu Rais Rigathi Gachagua akutana na wakurugenzi wa KTDA Jijini Nairobi.

Naibu Rais Rigathi Gachagua ameandaa mkutano na wakurugenzi wa Halmashauri ya Ustawi wa Majani Chai Nchini, KTDA katika makazi yake ya Karen jijini Nairobi.

Wakulima wa majani chai mwaka huu wanatarajia kupata mapato yaliyoimarika kufuatia mageuzi yaliyofanyiwa sekta hiyo ndogo.

Gachagua amekuwa akishinikiza kuimarishwa kwa sekta ndogo za kahawa na majani chai, ili kuboresha mapato ya wakulima katika sekta hizo.

Kupitia mtandao wake wa Twitter, Naibu huyo wa Rais alisema kuimarika kwa mapato hayo, kulitokana na ushirikiano wa mojamoja kati ya wakulima na wadau katika sekta hiyo.

Naibu Rais Rigathi Gachagua katika shamba la Majani Chai.

Gachagua alisema ataendelea kushirikiana moja kwa moja na wakulima 750,000 wa majani chai kote nchini, kuhakikisha wananufaika pakubwa na kilimo hicho.

 

Website | + posts