Naibu rais Rigathi Gachagua ameondoka hapa nchini Jumamosi alasiri, kuelekea Jijini Kigali, Rwanda, kuhudhuria kumbukumbu ya miaka 30 tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Katika ziara hiyo, naibu wa Rais anaongoza ujumbe wa Kenya unaojumuisha wabunge, katibu katika idara ya ughaibuni Roseline Njogu na viongozi wawili wa wanafunzi wa vyuo vikuu viwili.
Wanafunzi hao ni ustise Badali, rais wa chuo kikuu cha kiufundi cha Muranga na Ngugi Mwaura kiongozi wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Pwani.
Wabunge walioandamana na naibu wa Rais ni pamoja na naibu kiongozi wa wengi Owen Mbaya (Kilifi Kaskazini), Edward Muriu (Gatanga), Veronicah Maina (Seneta Mteule), Patrick Munene (Igamba Ngombe), Julius Rutto (Kesses), Parashina Samuel (Kajiado Kusini), John Kaguchia (Mukurwe-ini), Benjamin Langat (Ainamoi), Agnes Pareiyo (Narok Kaskazini) na aliyekuwa mbunge wa Charles Njagua Jaguar.
Gachagua pia anatarajiwa kukutana na wakenya wanaoishi nchini Rwanda katika hoteli moja, ambapo watajadili kuhusu kuboresha uwekezaji katika sekta zote zilizo kwenye ajenda ya kuimarisha uchumi wa taifa hili kupitia mfumo wa Bottom Up.