Home Habari Kuu Naibu Rais Gachagua kuhudhuria kongamano la kahawa nchini Colombia

Naibu Rais Gachagua kuhudhuria kongamano la kahawa nchini Colombia

0

Naibu Rais Rigathi Gachagua jana Jumapili usiku aliondoka nchini kuelekea Colombia ambako atahudhuria Kongamano la Wazalishaji na Wachomaji Kahawa Duniani litakaloandaliwa mjini Bogota. 

Baadaye, Gachagua atahudhuria mkutano wa viongozi wa kundi la nchi zinazoendelea, G77 utakaoandaliwa nchini Cuba.

Naibu Rais anasema azima ya kulainisha sekta ya kahawa nchini kwa manufaa ya mkulima daima inasalia imara.

“Ziara hii nchini Colombia itaongeza juhudi za kuifanya sekta ya kahawa kuwa ya manufaa kwa wakulima kama ilivyokuwa miaka iliyopita,” amesema Gachagua.

“Colombia ni nchi inayoongoza katika uzalishaji wa kahawa duniani. Inazalisha na kuuza kahawa katika mataifa kama vile Marekani, Ujerumani na Ubelgiji, mataifa ambayo Kenya inayalenga kupitia uongezaji wa thamani.”

Colombia inazalisha takriban asiilimia 12 ya kahawa inayozalishwa duniani, na kuifanya kuwa nchi ya tatu katika uzalishaji wa kahawa duniani.

“Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwao. Pia tumesaini mkataba wa maelewano na Colombia, ambao utsaidia kuimarisha uhusiano uliopo wa pande mbili,” aliongeza Gachagua.

Nchini Cuba, Naibu Rais atamwakilisha Rais Ruto katika mkutano wa viongozi wa G77 mjini Havana.

Website | + posts