Home Kaunti Naibu Rais Gachagua ahudhuria maombi kufariji waathiriwa wa ajali ya Londiani

Naibu Rais Gachagua ahudhuria maombi kufariji waathiriwa wa ajali ya Londiani

0

Naibu Rais  Rigathi Gachagua leo Jumanne, amejiunga na jamaa na marafiki pamoja na viongozi mbalimbali katika ibada ya kufariji familia za waathiriwa wa ajali iliyotokea katika eneo la Londiani juma lililopita.

Takriban watu  54 walifariki huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika ajali hiyo, iliyotokea siku ya ijumaa. Ibada hiyo ya maombi  iliyoongozwa na viongozi wa makanisa mbalimbali, iliandaliwa mjini Londiani.

Awali, Gachagua alituma risala za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na kwa wakenya kwa jumla kupitia ujumbe wa twitter.

Siku ya Jumatatu, serikali ilisema kuwa itawasaidia waathiriwa na familia zilizowapoteza wapendwa wao, katika ajali hiyo ya Londiani.

Gavana wa kaunti ya Kericho  Dkt. Eric Mutai, alitoa hakikisho kuwa serikali ya kaunti hiyo italipa gharama za hospitali na zile za makafani kwa waathiriwa wa ajali hiyo.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here