Home Kimataifa Naibu Gavana wa Lamu Raphael Munyua Ndung’u amefariki

Naibu Gavana wa Lamu Raphael Munyua Ndung’u amefariki

Kiongozi wa taifa alisema, naibu huyo Gavana alileta mabadiliko makubwa yaliyoimarisha maisha ya wakazi wa kaunti hiyo.

0
Naibu Gavana wa Lamu Raphael Munyua Ndung’u.
kra

Naibu Gavana wa kaunti ya Lamu Raphael Munyua Ndung’u, amefariki.

Kupitia mtandao wa X, Rais William Ruto amemuomboleza naibu huyo Gavana, akimtaja kiongozi aliyejitolea kuwahudumia wananchi.

kra

Kiongozi wa taifa alisema, naibu huyo Gavana alileta mabadiliko makubwa yaliyoimarisha maisha ya wakazi wa kaunti hiyo.

“Nimehuzunishwa na habari za kifo cha Naibu Gavana wa Lamu Raphael Munyua Ndung’u. Alikuwa kiongozi mwenye maendeleo, aliyefanyakazi kwa bidii kuimarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo,” alisema Rais Ruto.

Rais pia alituma rambirambi kwa familia, marafiki na jamii nzima ya Lamu, akiwahakikishia kuwa taifa linawaombea wakati huu mgumu wa majonzi.

“Tunawaombea familia, marafiki na wakazi wote wa Lamu kwa jumla, wakati huu wa huzuni,” aliongeza Rais Ruto.

Website | + posts